Waweza Kuwa kituko, Ugeuke kichekesho
Wakati mtu mzuri, Penzi likakubadili
Sumu nilioimeza, Sijui ni sumu gani
Nimefanya naloweza, Na bado ni taabani
Nimeshakunywa maziwa, Sumu sijaitapika
Akili haifikiri, Nimekumbwa kitu gani
Nina zunguka zunguka, Ninatembea tembea
Ninaongea ongea, Na hata sijielewi
Au nimekuwa teja, teja wa mapenzi
Oooh Nimebwia unga , ooh sijiweza
Mimi nimekuwa teja, teja wa mapenzi
Huu nilobwia unga, sijui aina gani
Kumbe mapenzi ni sumu, kumbe mapenzi uteja
Hasa yakiwa magumu, unageuka kioja
Na mimi sijifahamu, nimeenda kila rehab
Nikipona narudia, na kuyaacha nimeshindwa
Nina zunguka zunguka, ninatembea tembea
Ninaongea ongea, na hata sijielewi
Mimi nimekuwa teja, teja wa mapenzi
Oooh nimebwia unga , ooh sijiwezi
Mimi nimekuwa teja, teja wa mapenzi
Huu nilobwia unga, sijui aina gani
Nilidhani natafuta faraja, na kumbe nina anguka (kwenye uteja)
Zungu linipa maradhi iiiiiiiih iiih, maradhi
Na bado nalizimia, tena sana
Pesa zenyewe hakuna, Na bado nakimbilia
Kumbe mapenzi uteja, uteja
Kumbe nimekuwa teja , teja wa mapenzi
Jamani nimebwia unga, ooh sijiwezi
Mwenzenu nimekuwa teja, teja wa mapenzi
Sijui nilobwia unga, sijui aina gani
Teja ni hoi taabani, teja wa mapenzi
Teja ni hoi kitandani , oooh sijiwezi
Kumbe nimekuwa teeeja, teja wa mapenzi
Kumbe nimekuwa teja aah, Sijui aina gani
----