Waptrick Sajna - Mganga Song Lyrics

 • Ooh mganga, mganga wee,

  Ooh mganga, mganga wee,

  nahitaji msaada, mganga wee,

  Ooh mganga...

  VERSE-1 (SAJNA)

  Mi mcha Mungu wala si mshirikina, walimwengu mnieleweee,

  niko timamu hata uchizi sina, ni moyo unachotaka upewe,

  uzuri wake zaidi ya hadhi ya ikulu,

  ntampataje mi mwenyewe mtoto wa Kasulu haa,

  uzuri wake zaidi ya hadhi ya ikulu,

  ntampataje mi mwenyewe mtoto wa Kasulu haa,

  nimejaribu njia zote na hii ndo ya mwisho, haa ng'wana waneee, nimechukua za mbayuwai nimeongeza na zangu, haa ng'wana waneee,(ng'wana wanee)

  CHORUS (SAJNA)

  Hodi hodi hodi mganga, jina langu Saj kwako nimetinga,

  nachohitaji unifanyie manyanga, kwa yule binti mi ninayempenda,

  Hodi hodi hodi mganga, jina langu Saj kwako nimetinga,

  nachohitaji unifanyie manyanga, kwa yule binti mi ninayempenda,

  VERSE-2 (SAJNA)

  Kwanza nachohitaji mganga,

  anapokuja kwangu awe na khanga (yeeah),

  nikikutana naye barabarani (mamaa),

  nikimuita basi aache kuringa (na),

  aniombe ndoa mimi mtoto wa mtaa,

  na mahari atoe yeye (mwenyewe),

  ntakupa mali zote hata nilale njaa,

  ufanye nimpate yeye (we mganga),

  na na na na mgangaaaaa aaaah ah,

  REPEAT CHORUS (SAJNA)

  VERSE-3 (JOSEFLY)

  Horai horai horai tabuu,

  wameshaskia skia wakuu,

  songa mpaka ndani kwanza toa viatu kwa miguu,

  usiwe na wasi hapa umefika na utampata tuu,

  hii dunia ni yetu lakini wachache tunaijua,

  na wao mabinti wazuri wazuri ni wa kwetu tumeumbiwa,

  mi nauwezo wa kuibadili mbalamwezi ikawa jua,

  ni mtoto wa mwana mpolimpolimo,na wale wa kale wakolikolimo,

  wakaja waganga wabolibolimo na,namimi nimonimo,

  niskize Sajna una nyota ya kichaga ila una moyo wa kichina,

  huyu binti amefanya moyoni umekosa stamina,

  usijali umeshampata ila ukifanya nachosema, leta

  leta kucha za huyo binti alizokata kwa meno,

  nywele za kikwapa na harufu yake umenipata,

  (SAJNA)

  Ntapata vipi na mwenyewe anaringa,

  hata nikimwita kitaani ananipinga,

  Ntapata vipi na mwenyewe anaringa,

  tafadhali mganga sema kingine tena,

  (JOSEFLY)

  Nenda ulete sabuni ambayo tayari ameogea,

  kijana fanya fastafasta kabla giza kuingia,

  leta bra anayovaa pindi anapozima taa,

  nyayo za miguu za marehemu babu aliyemzaa,

  kope za macho yake anapoanza kusinzia,

  nahitaji nywele zake na alama y viganja pia,

  umeniskia, hapa atakuja tu kubembeleza umwite dear, umwite dear,

  REPEAT CHORUS (SAJNA)

  VERSE-4 (SAJNA)

  Ntajaribu kufanya lolote, ili mimi nimpate yeye,

  niko tayari hata kukatwa ulimi,ilimradi mi niwe na yeye,

  kama ni kope zake, ama na kucha zake,nitaongea na rafiki zake,

  kama ni kope zake, ama na kucha zake,nitaongea na rafiki zake,

  kuna vingine mi nashindwa mganga,hapo itabidi unielewe,

  kama ni pesa nitaongeza mganga,ili vingine ufanye wewe,

  ooh mganga, ooh mganga

  nahitaji msaada, msaada

  ooh mganga, mganga we

  ooh hii ooh oh oh (mganga we) (4x)

  lalalalalalalalalalala mganga we),

  ooh hii ooh oh oh (mganga we),

  lalalalalalalalalalala (mganga we),

  ooh hii ooh oh oh (mganga we)

 • Sajna other songs
 • Lyrics Search
 • Videovak Watch Free
  VIDEOVAK: Watch TV series online free!
 • Waptrick Home Page
 • Change Language