waptrick.com

Waptrick Wanaume Kama Mabinti - Lady Jay Dee Song Lyrics


Chorus

Mnakula kunywa na kuvaa, siku zinaendaa

Vya bure hupenda kupewa, wala hamna fikira

Kila upande mnafiti, siku zinaenda

Vinywa vimejaa ufitini, wanaume kama mabinti

Verse 1 -

Lady Jaydee

Ninavyosema wanaume simaanishi woteella wale ye tabia kama za mabinti

Utawaona kwenye magari ya mademu zao

Wakitanua na kucheka, utadhani yao

Hupenda kuwaliwaza wamama, watu wazima

Hawana mapenzi ya kweli, moyoni wanawaza pesa

Nikisema wanajiuza, katu sitokosea

Tutawatofautishaje hawa na machangudoa

Repeat Chorus

Verse 2 -

A-Y

Sema sema sema, haki yako Jaydee

Tembo kuvaa vipusa, haki yako ni halali zaidi

Siwezi danganya, sina upendo upande mlipo marafiki

Ndugu aa mwisho wa wiki, hatuwezi kuwa washkaji

Kama una moyo wa plastik, Ambwene aliona

Usoni kama watu, mioyoni unafiki mtupu

Siyo kula siyo kuvaa tegemezi mpaka mkwanja wa kondomu

Sikufahamu hii ni simple zaidi ya kumnyatia kiziwi

Wanaume gani hawaelewi mambo ya kiume

Nataka muache kutazama, nataka muone

Mnajidanganya wenyewe na inakolea zaidi ya mnapodanganya wengine

Sizuii msifanye mfanyayo

Tunafikiria kwa ubongo, siyo kwa nyayo

Inshaalla inshaalla kibao maisha kuwafuata mbio

Ujinga huo kusanya mawazo yenu na ninaacha mungu awahukumu

Binamu

Repeat Chorus

Verse 3 -

Lady Jaydee

Ukiwakuta kwenye vikao vya pombe

Eti wao wasemaji wanaojua yote

Kumbe hatoi hata senti ya kulipa bili

Ikifika zamu yao huenda msalani

Kwa ukuwadi wao namba moja hupenda

Wanapenda kuwaliwaza mademu wa wenzao

Shoga zangu hebu leteni magauni tuwavishe

Hijabu tuwafunge na vimini vitopu tuwaazime

Repeat Chorus

Verse 4

Umeona wapi

Wanaume kunyweshwa pombe

Hivi tangu lini dume likasutwa

Umesikia ya jana

Hassan naye kaja Kitchen Party

Mwanishangaza!

Repeat Chorus

----
» Lady Jay Dee other songs
« Lyrics Search
« Waptrick Home Page
« Change Language
» Download free VPN for iPhone